Ni kwa fahari na uwajibikaji mkubwa nakuletea ujumbe huu kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi ya National Enterprise and Development Chamber (NEDC). Chama hiki kimeanzishwa wakati ambapo ari ya ujasiriamali nchini Tanzania haiwezi kupuuzwa, huku pengo katika mfumo wa mazingira ya biashara limewaacha vijana wengi na biashara zenye matumaini bila nafasi ya kukua.
Tunataka kuwahakikishia wadau wote—serikali, washirika wa maendeleo, sekta binafsi, na wanachama wetu— kwamba NEDC imejengwa juu ya misingi ya uwazi, uadilifu, na uwajibikaji. Bodi ya Wakurugenzi imeundwa ili kuhakikisha taasisi hii inazingatia viwango vya juu vya utawala bora.
Kwa wanachama wetu, NEDC ni nyumbani halisi. Kwa washirika na wafadhili wetu, NEDC ni mahali salama— jukwaa ambalo rasilimali zinatumiwa kwa uadilifu, weledi, na matokeo yanapimwa kwa uaminifu.
Kwa utawala kama huu, tunaweza kusema kwa kujiamini kwa wadau wetu wote: kushirikiana na NEDC ni uwekezaji katika mustakabali wa Tanzania ambao ni salama na wenye tija. Kwa niaba ya Bodi, ninathibitisha tena wito wetu wa kuiongoza taasisi hii kwa hekima, uwajibikaji, na maono. Pamoja na Timu ya Utendaji, tutaakikisha NEDC inatimiza majukumu yake, inatoa matokeo halisi, na inakuwa nguzo ya maendeleo ya biashara kwa vizazi vijavyo.
Benedict Ishabakaki
Mwenyekiti wa Bodi
Ninapotembea mitaani kwenye miji yetu na maeneo mbalimbali, nnaona ukweli ambao unaniathiri na kunipa tumaini. Naona ubunifu, bidii, na kipaji cha vijana wetu. Naona pia jinsi uwezo huo unavyopotea—si kwa ukosefu wa nia, bali kwa sababu ya pengo katika mfumo wa mazingira ya ujasiriamali.
National Enterprise and Development Chamber (NEDC) ilizaliwa kutokana na imani: kwamba hakuna kipaji kinachopaswa kupotea, na hakuna mjasiriamali anayepaswa kumwagiwa baridi kwa kukosa msaada. Tupo hapa kufunga pengo— kuwaunganisha waliokuwa na fursa na wasiokuwa nazo katika harakati moja ya biashara, ubunifu, na maendeleo ya taifa.
NEDC si chama tu. Ni jukwaa, ni sauti, na ni familia kwa wajasiriamali wa tabaka zote. Tupo kuwaunganisha na fedha, masoko, mafunzo, ushauri, na sera zinazoweza kufungua ukuaji wao.
Tunapoanza safari hii, dhamira yetu ni rahisi lakini thabiti: kuunda Tanzania ijayo—ambapo biashara ndiyo injini ya ustawi, nafasi zinapatikana kwa wote, na mawazo ya vijana wa leo yanakuwa makampuni ya kesho.
Hati hii ni zaidi ya nyaraka. Ni mwaliko—kwa serikali, washirika wa maendeleo, wawekezaji, na wananchi—kuungana nasi kujenga Taifa ambapo hakuna ndoto inayopotea na hakuna mjasiriamali anayesahaulika. Pamoja, tunaweza kubadilisha uwezo kuwa matokeo, na matumaini kuwa athari endelevu.
— Jesse Stephen Madauda
Mwanzilishi & Mkurugenzi Mtendaji